Search This Blog

Friday, December 20, 2019

Kiungo Prisons azisikilizia Simba, Yanga

Licha ya kuhusishwa kuwaniwa na timu za Simba na Yanga, kiungo wa Prisons, Cleoface Mkandala amesema hakuna hata moja kati ya hizo mbili ambayo imefanya mazungumzo naye rasmi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkandala alisema kuwa amekuwa akisikia taarifa za kuhitajika na timu hizo lakini hazijafanya mawasiliano yoyote rasmi na uongozi wake ama yeye mwenyewe.

“Hakuna ukweli wowote juu ya mimi kujiunga na moja kati ya timu hizo kwa sasa kwani sijafanya mazungumzo yoyote nao na wala hawajazungumza na timu yangu ambayo bado nina mkataba nao.

“Baada ya mashindano ya Chalenji kumalizika, sasa narejea katika klabu yangu lakini dirisha la usajili ndio kwanza limefunguliwa hivyo lolote linaweza kutokea iwe kubaki au kuondoka lakini itategemeana na maridhiano ambayo yatafikiwa na timu itakayonihitaji pamoja na muajiri wangu.

“Sipendi sana kuziamini tetesi kwa sababu zinaweza kumvuruga mchezaji kisaikolojia. Napenda kufuata taratibu katika kila jambo ninalofanya mwaka huu,” alisema Mkandala

Mkandala amekuwa gumzo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kutokana na uwezo mkubwa wa kupiga pasi zinazozaa mabao ambapo hadi sasa ameshafanya hivyo mara nne.

Advertisement

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...