Search This Blog

Friday, December 20, 2019

Mgunda ajivunia vijana Chalenji

By Charles Abel

Licha ya timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kumaliza ikiwa nafasi ya nne katika mashindano ya Chalenji, kocha Juma Mgunda ametamba kuwa wachezaji wake vijana wamepata uzoefu wa kutosha na kuimarika katika mashindano hayo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mgunda alisema kuwa baadhi ya wachezaji wake hawakuwahi kucheza mechi za kiushandani wakiwa na jezi ya timu ya taifa lakini pamoja na hilo hawakuonyesha tofauti kubwa na wengine katika mashindano hayo.

“Vijana wamecheza vizuri ukizingatia hii ni mara ya kwanza kwao kupata nafasi ya kucheza mechi za ushindani wa kimataifa hivyo kile walichokifanya ni kikubwa na wanastahili pongezi na naamini huu ni mwanzo mzuri kwao.

“Tunaelekea katika Fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) na hapa tumecheza mechi tano zenye ushindani ambazo katika hali ya kawaida tusingeweza kupata michezo mitano ya kirafiki kutokana na gharama na kubana kwa ratiba.

Hivyo uzoefu huu walioupata ni fursa muhimu na kubwa kwao kupiga hatua kisoka lakini wanatakiwa kuendelea kujituma na kujiweka fiti zaidi ili waendelee kupata nafasi kikosini ukizingatia kwamba tuna kundi kubwa la wachezaji vijana ambao wamekuwa wakifanya vyema na kila mmoja ana hamu ya kuchezea timu ya taifa,” alisema Mgunda.

Wachezaji ambao kwa mara ya kwanza wameanza kuvaa jezi za timu ya taifa katika mashindano hayo ni Lucas Kikoti (Namungo), Mwaita Gereza (Kagera Sugar), Baraka Majogoro (Polisi Tanzania), Cleoface Mkandala (Prisons), Eliuter Mpepo (Buildcon), David Kisu (Gor Mahia), Nickson Kibabage (Difaa El Jadida) na Paul Nonga (Lipuli).

Advertisement

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...