Search This Blog
Thursday, November 28, 2019
Serikali kutumia wataalamu wa ndani kutekeleza miradi
Ezekiel Mtonyole-Mpwapwa
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa, amesema wamekusudia kuanzia Sasa kuanzisha utaratibu wa kutokutumia wakandarasi au kutoa tenda katika miradi ya maji inayotekelezwa maeneo mbalimbali hapa nchini na badala yake watatumia wataalamu wa ndani ya Mamlaka za maji kukamilisha miradi hiyo.
Waziri Mbarawa ametoa kauli hiyo Wilayani Mpwapwa wakati wa ziara yake Wilayani Mpwapwa kukagua utekelezaji wa miradi ya Maji, ambapo amesema wamefikia hatua hiyo baada ya wakandarasi wengi kuchukua fedha na kutokukamilisha miradi hiyo, amesema serikali imewekeza fedha nyingi Sana lakini matokeo yake hayaonakani.
Na kubainisha kuwa miradi mingi wanapewa wakandarasi ambao hawana uwezo au kupeana tenda kindugu na kutekeleza miradi chini ya kiwango.
"Serikali za awamu zote zilizopita ilitenga fedha nyingi Sana kwa ajiri ya miradi ya maji lakini matokeo yake hayaonekani wote tunajiuliza fedha zinakwenda wapi wakati maji hayatoki na fedha hazirudishwi na majibu yake kila mtu anayo"
"Kwahiyo tumeamua kuja na utaratibu huu wakuto kuwatumia wakandarasi na badala yake tutatumia wataalamu wa ndani ya Mamlaka zetu za maji na mfano tumefanya hivyo Mkoa wa Katavi na matokeo tumepata" amesema Waziri Mbarawa.
Katika Ziara hiyo Wilayani Mpwapwa ametembelea miradi ya maji Luhundwa na Bumila kuona utekelezaji wake wake na akiwa katika mradi wa Maji wa Bumila, Waziri wa Mbarawa amewahakikishia wananchi wa Kata hiyo kuwa hivi karibuni wataanza kupata huduma ya maji Safi.
Kwani mradi huo ulikwama kutokana na mkandarasi kutolipwa fedha lakini kwa Sasa mkandarasi huyo kashalipwa fedha na mradi huo utakamilika ndani ya mda mfupi na wataanza kupata huduma ya maji.
"Tunajua mkandarasi wa mradi huu alisimama lakini tumeshamlipa fedha zake na atakuja kukamilisha mradi huu, pia nishukuru Chama Cha Mapinduzi waliweka pumpu ya dharura na mkawa mnapata huduma ya maji, Sasa tutapanua zaidi na kuongeza vituo zaidi ili mpate huduma ya maji kikamilifu naomba muiamini serikali yenu" amesema.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akitoa taarifa ya Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Binilith Mahenge, amesema licha ya miradi mingi kutokukamilika lakini bado huduma ya maji inazidi kuimarika kwani mwaka 2015 ni asilimia 43 tu ndio walikuwa wakipata huduma ya maji na Sasa ni asilimia 57 kwa miji midogo na Wilaya.
Wakati kwa miji mikubwa upatikanaji wa maji ilikuwa, ni asilimia 65 na Sasa ni asilimia 82, na wamejipanga angalau kufikia mwaka 2025 kwa miji midogo ifikie asilimia 80 na miji mikubwa wafikie asilimia 95.
Aliongeza kuwa " kwa Wilaya ya Mpwapwa Kuna miradi 10, inayotekelezwa mpaka Sasa, Saba (7)mipya na mitatu(3) ya ukarabati yote ikiwa na thamani ya shilingi bilioni 4.17, huku changamoto ikiwa ni fedha kutofika kwa wakati maeneo husika" amesema DC Shekimweri.
Kutokana na hali ya kutofika kwa wakati kwa fedha za utekelezaji wa miradi hiyo Mkuu huyo wa Wilaya amemuomba Waziri kuhimiza watendaji wa Mamlaka za maji na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA makao makuu kupeleka fedha kwa wakati ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati wananchi waweze kupata huduma ya maji Safi.
Amesema changamoto hiyo ya fedha kutofika kwa wakati imekuwa chanzo kikubwa kwa miradi mingi kutokamilika kwa wakati katika Wilaya hiyo huku wananchi wakiendelea kupata adha ya maji.
Baadhi ya Wananchi wa wanaozungua mradi wa Maji wa Bumila wameishukuru serikali kwa kuleta fedha za mradi huo kwani shida ya maji katika eneo hilo ni kubwa sana wamesema angalau Sasa adha ya maji itapungua kwa kiasi kikubwa Sana kwani hiyo ilikuwa kero kubwa Sana kwao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment