Search This Blog

Thursday, November 28, 2019

Waziri Ndalichako azindua chuo kipya cha VETA Kagera


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amezindua chuo kipya cha VETA Ndolage kilichopo Kamachumu Wilaya ya Muleba mkoani Kagera kilichokamilishwa kwa Shilingi milioni 281.

Ujenzi wa Chuo hicho ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya kushirikiana na Jamii kufikisha Elimu ya Ufundi karibu na Wananchi pamoja na kujenga Vyuo vya VETA katika kila Wilaya nchini ifikapo mwaka 2020.

Wizara imetenga zaidi Bilioni 40 katika mwaka wa fedha 2019/20 kwa ajili ya ujenzi wa Vyuo vya VETA vya Wilaya 25 nchini.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...