Search This Blog
Saturday, October 26, 2019
Watatu kizimbani kwa wizi wa tausi watatu wa Ikulu
Serikali imewafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu watu watatu kwa kosa la kukutwa na tausi watatu wanaodaiwa kuwa wa Ikulu.
Washtakiwa hao ni David Graha, Mohamed Hatibu na Mohamed Ally, wamefikishwa mahakamani hapo leo Ijumaa Oktoba 25, mbele ya Hakimu Mkazi Vicki Mwaikambo.
Wakili wa serikali Mkuu Faraja Nchimbi akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon, wamedai washtakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya Julai Mosi mwaka 2015 hadi Oktoba 14, mwaka huu jijini Dar es Salaam
Inadaiwa kuwa katika kipindi hicho, washtakiwa hao walijihusisha na kuratibu mtandao wa uhalifu kwa kujihusisha na biashara ya ndege aina ya tausi bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Ambapo imedaiwa katika kipindi hicho, washtakiwa walikutwa na tausi watatu wenye thamani ya Dola za Marekani 1500 sawa na Sh 3,444,150 mali ya serikali bila ya kibali.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Hakimu aliwataka Washtakiwa hao kutojibu lolote kwakuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Kesi itatajwa tena Novemba 7 mwaka huu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment