Search This Blog
Saturday, October 26, 2019
Mama Diamond aomba ‘Uno’ ya Harmonize, Diamond acheza ya Ali Kiba, Rich Mavoko
Bosi wa WCB, Diamond Platinumz ameonesha kwa vitendo kuwa biashara yake ya Radio na Televisheni ni kwa ajili ya wote bila kujali uhusiano wake binafsi na msanii anayetajwa.
Jana, alichukua nafasi ya kuwa mtangazaji na mcheza santuri (DVJ) wa kipindi kimojawapo akiwataka watazamaji kuchagua nyimbo wazipendazo na yeye alizitendea haki akifuata matakwa ya watazamaji.
Akionesha moja kwa moja kupitia ‘Insta Live’ akiwa ndani ya Wasafi TV, alikutana na shabiki wa Harmonize, Mama Dangote ambaye ni mama yake mzazi aliyeomba wimbo mpya wa mwanafamilia huyo wa zamani wa WCB ambaye amejitoa na kuanzisha ‘Konde Gang’.
Hata hivyo, Diamond alishindwa kucheza wimbo huo akitoa maelezo kuwa hauna video hadi sasa lakini alimpa mtazamaji ladha nyingine kutoka kwa Harmonize, ‘Shulala’ aliyomshirikisha Korede Bello.
Alisoma ujumbe mwingine wa shabiki aliyeomba wimbo wa Ali Kiba, ‘Aje’ na mwingine aliomba wimbo wa Rich Mavoco ‘Kokoro’.
Ingawa baadhi ya watu wanahisia kuwa hana maelewano mazuri na wasanii hao, alizicheza nyimbo hizo akisisitiza kauli mbiu ya kituo hicho cha TV, ‘Hii ni Yetu Sote’.
Mavoko alijitenga na WCB akilalamikia kuwa mkataba aliokuwa ameingia nao ni haukuwa unamtendea haki. Kadhalika, Harmonize juzi ameeleza kuwa ilimbidi auze nyumba zake tatu kukamilisha vigezo vya kuvunja mkataba wa WCB ambapo alitakiwa kulipa Sh. 500 milioni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment