Search This Blog

Sunday, October 20, 2019

TANZIA: Mwanzilishi wa Babati Half Marathon afariki dunia



Na John Walter-Babati

Pigo kubwa wamepata wakazi wa mji wa Babati na mkoa mzima wa Manyara baada ya kuondokewa na mfanyabiashara mkubwa mkoani humo na  Mwanzilishi wa Babati Half Marathon.

Taarifa iliyotolewa na mtu wa karibu na familia ya marehemu Mbunge wa Babati Vijijini Vrajil Jituson,Inasena kuwa Mfanyabiashara huyo mwenye asili ya Asia amefariki dunia Majira ya mchana jana Oktoba 19.2019 wakati akipatiwa Matibabu  katika Hospitali ya Selian Jijini Arusha.

Jituson amesema Mwili wa marehemu mzee Bajwa utazikwa leo saa saba mchana katika majaburi ya Njiro Jijini Arusha.

Marehemu alikuwa nguzo muhimu katika kusapoti maendeleo ya mchezo wa riadha mkoani Manyara kwani ndiye alieanzisha mashindano ya riadha maarufu kama Babati Half Marathon yanayofanyika January Mosi ya kila mwaka.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi,Amina.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...