Search This Blog

Sunday, October 20, 2019

Wabunge wa Uingereza wapiga kura kuchelesha Brexit

Wabunge wa Uingereza wameunga mkono marekebisho ya mpango wa taifa hilo kujiondoa katika Umoja wa Ulaya-Brexit wa Waziri Mkuu Boris Johnson, hatua ambayo itamlazimisha kuchelewesha hatua ya kujiondoka katika umoja huo.

Bunge hilo limepiga kura 322 kwa 306 kwa marekebisho ya kuzuia kwa muda mfupi, makubaliano hayo ambayo yaliridhiwa siku chache zilizopia mjini Brussels.

Hatua hiyo inamaanisha mpango huo hauwezi kuridhiwa mpaka utekelezaji wa sheria ufanikiwe kupita Bungeni.

Kiongozi wa upinziani Jeremy Corbion amesema waziri mkuu sasa lazima afuate sheria na kuomba kuongezewa muda wa Brexit kutoka Umoja wa Ulaya.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...