Search This Blog
Wednesday, October 16, 2019
Sehemu ya Bweni la Korogwe Girls lateketea kwa moto
Bweni la Shule ya Sekondari ya Wasichana (Korogwe girl) limeteketea kwa moto na kusababisha vifaa vya wanafunzi kuteketea kwa moto.
Kwa mujibu wa Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Korogwe girls, Anisia Mauka, moto huo umeteketeza sehemu ya bweni la Amani ambalo linatumiwa na wanafunzi wa kidato cha tatu na cha kwanza wakati wanafunzi wakiwa darasani wakijisomea.
Mwalimu huyo amesema, jumla ya vitanda 38 na magodoro yake pamoja na masunduku ya wanafunzi hao yameteketea kwa moto uliotokea jana usiku.
Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na hakuna vifo vilivyotokea isipokuwa kuna wanafunzi 12 ambao walipata mshtuko lakini wakapatiwa matibabu katika Hospitali ya Magunga na majengo na kwa sasa wanaendelea vizuri na wameruhusiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Kai...



No comments:
Post a Comment