Search This Blog
Wednesday, October 16, 2019
RC Kilimanjaro atoa magari kwa CCM na CHADEMA
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ameagiza vyama vya siasa mkoani humo vipewe gari ili wazunguke kuhamasisha wananchi wajitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura Uchaguzi serikali za mitaa.
Vyama hivyo ni pamoja na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Sauti ya Uma (SAU).
Ametoa maagizo hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Matadi, kata ya Endumeti Wilayani Siha ikiwa ni siku ya pili ya uhamasishaji kwa wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura mkoani Kilimanjaro.
Maagizo haya yamefuatia hoja iliyotolewa leo na Azaria Mdoe aliyekuwa Mgombea ubunge wa jimbo la Siha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama cha Sau.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment