Search This Blog

Thursday, October 10, 2019

Marekani: Wakuta dawa za kulevya ufukweni wakiwa likizo


Familia moja ambayo ilikuwa likizoni katika pwani ya jimbo la Marekani la South Carolina ilishangaa wakati walipota kifurushi kutoka baharini chenye dawa ya kulevya aina ya cocaine zenye thamani ya dola za Kimarekani 600,000.

Vyombo vya habari vimemnukuu afisa wa polisi, Bob Bromage akisema kwamba familia hiyo ilikuta kifurushi hicho kikielea karibu na pwani ya Kisiwa cha Fripp Jumapili usiku.

Familia hiyo walichukua kifurushi hicho chenye uzito wa kilo 20 na kupata matofali ya poda nyeupe ndani. Baadaye polisi walitabua kuwa poda nyeupe ilikuwa cocaine, yenye bei ya soko ya karibu dola 600,000.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...