Search This Blog
Thursday, October 10, 2019
Rais Magufuli awaonya wakimbizi wanaojihusisha na ujambazi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amewataka wakimbizi kutoka nchini Burundi ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kigaidi hapa nchini kuacha mara moja.
Rais Magufuli ametoa onyo hilo alipokuwa akizungumza na wananchi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi baada ya kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Mpanda hadi Tabora na kuzindua kituo kipya cha mabasi kilichopewa jina la Waziri Mkuu msataafu, Mizengo Pinda.
“Katika mkoa huu kuna wenzetu kutoka Burundi na maeneo mbalimbali ambao tuliwakaribisha katika nchi yetu kama Tanzania ilivyo na ukarimu kwa watu kutoka nje lakini pamejitokeza baadhi ya changamoto watu wako kambini baadhi yao wakawa wanashiriki katika masuala ya ujambazi kulifanya eneo hili lisiwe salama kwasababu ya ukarimu wetu,”
“Hauwezi ukakaribishwa kwasababu ya shida ulizozitengeneza huko kwenu uje uzilete hapa hivyo nitoe wito kwa ndugu zetu ambao walikuja hapa tukawapokea kwa upole wasije wakalifanya eneo hili likawa la hatari,”
“Hamuwezi mkakaribishwa halafu baadhi yenu wanashiriki kuwaonea raia wema na saa nyingine kupitisha silaha kupitia Ziwa Tanganyika ninawaomba waache na kutokana na mienendo hiyo ambayo haifurahishi tumeona tulichunguze hili suala la kuwapatia uraia watoto wao kwasababu wanaweza wakaleta watu wakasema ni watoto wao kumbe ni majambazi kwani wamekuwa na tabia ya kukaribisha wenzao wiki hii yuko hapa wiki inyokuja yuko Burundi na kadhalika,”
Aidha amewataka Watanzania kuacha kuishi na raia hao wa kigeni kwa misingi kwamba wanawasaidia katika kazi kwasababu wao wanakuwa wanawasoma halafu usiku wanakuja, Tanzania ni nchi ya amani na palipo na amani kunakuwa na kila kitu,” amesema Rais Magufuli.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment