Tunisia inatarajiwa kufanya uchaguzi wa rais leo. Hii itakuwa mara ya pili kwa nchi hiyo kufanya uchaguzi huru wa rais kwa njia ya demokrasia tangu kutokea vuguvugu lililotokea mwaka 2011 na kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Zine el-Abidine Ben Ali.
Wagombea 26 akiwemo Waziri Mkuu Youssef Chahed watashiriki uchaguzi huo. Hata hivyo haijajulikana wazi ni nani atafaulu kuingia kwenye duru ya pili ya uchaguzi huo.
Wapiga kura milioni saba wanatarajiwa kushiriki uchaguzi huo, baada ya kumalizika rasmi kampeni zilozojikita zaidi kwenye changamoto za kijamii na kiuchumi zinazoizonga nchi hiyo ya Afrika kaskazini.
Hapo jana, wagombea wawili waliamua kujitoa kwenye uchaguzi huo na badala yake kumuunga mkono waziri wa ulinzi Abdelkarim Zbidi.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment