Search This Blog

Sunday, September 15, 2019

Fahamu Sababu za Mwenyekiti Simba Kujiuzulu



Leo Septemba 14, 2019 uongozi wa klabu ya Simba umetoa taarifa kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Swedi Mkwabi amejiuzulu nafasi yake.



Taarifa hiyo imeeleza kuwa Swedi ameiandikia Barua Bodi ya Wakurugenzi kupitia kwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mohammed Dewji, ambapo ameeleza sababu kuu ya kijiuzulu nafasi hiyo ni kuhitaji muda zaidi kusimamia shughuli zake binafsi.

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba pamoja na Sekretarieti ya Simba imemtakia kila la heri katika shughuli zake.

Lakini pia imeeleza kuwa ina imani ataendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za klabu kama ilivyokuwa awali kabla kupata nafasi hiyo.

Aidha imebainisha kuwa utaratibu wa kumpata Mwenyekiti mpya utatangazwa.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...