Search This Blog
Monday, September 2, 2019
Teknolojia ya habari na mawasiliano ina nafasi kubwa - Dk. Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kwamba teknolojia ya habari na mawasiliano ina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko ya maendeleo katika Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola.
Rais Dk. Shein aliyasema hayo katika ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Chama Cha Mabunge cha Jumuiya ya Madola (CPA) Kanda ya Afrika unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinatul Bahr, iliyopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Rais Dk. Shein alisema kwamba iwapo teknolojia ya habari na mawasiliano itatumika ipasavyo hasa katika kuimarisha kanzi data mbali mbali hatua hiyo itarahisisha suala zima la kufanya maamuzi kwa wakati na kuweza kufikia malengo yaliokusudiwa.
Aliongeza kuwa uendeshaji wa Bunge kwa kutumia njia za kisasa kunawaweka karibu zaidi Wabunge na wananchi, jambo ambalo linatoa fursa pana zaidi kwa wananchi ya ya kutoa maoni yao na hoja mbali mbali za maendeleo zinazogusa maisha yao ya kila siku.
Alieleza kuwa Bunge Mtandao ni nyenzo nzima ya kupunguza harama za mambo mbali mbali kama vile usafiri sambamba na kuokoa muda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment