Search This Blog
Monday, September 2, 2019
Tembo wavamia makazi ya watu na kula chakula
Jumla ya kaya 11 katika kijiji cha Halawa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, hazina chakula wala mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuvamiwa na tembo na kuharibiwa vibaya.
Licha ya nyumba hizo kuharibiwa, tembo hao pia wamekula chakula chote kilichohifadhiwa ndani ya nyumba hizo.
Tembo hao zaidi ya 10 waliotoka katika pori la akiba Maswa, wanadaiwa kuvamia kijiji hicho usiku wa kuamkia jana Septemba Mosi, saa saba usiku, ambapo waliezua nyumba 11 za familia saba zenye watu zaidi ya 50.
Mmoja wa wananchi walionusurika na kadhia hiyo, Mwalu Nsulwa amesema tembo hao walivamia kwenye nyumba yake na kula mahindi yote gunia tano na viazi vilivyokuwa vimehifadhiwa ndani.
“Baada ya tembo kuvamia walianza kula mahindi na viazi vyote wakamaliza na wameezua hadi nyumba na sasa sina sehemu ya kuishi.
“Wakati wanaingia mimi na watoto wangu wawili tulijificha uvunguni mwa kitanda ili kunusuru maisha yetu,” amesema Nsulwa.
Aidha, Mtendaji wa kijiji hicho Mayenga Matongo amesema tembo hao walivamia kaya saba na kuezua nyumba zote 11 na kula mahindi magunia 42, viazi magunia sita huku akibainisha kuwa hakuna vifo vilivyotokea.
“Familia hizi hazina sehemu ya kulala tena maana nyumba zao zimeharibiwa vibaya, hawana hata chakula kutokana na kuliwa na tembo na kilikuwa kimehifadhiwa ndani ya nyumba zao,” amesema Matongo.
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Festo Kiswaga akiwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya, walifika eneo la tukio na kutoa pole kwa wananchi hao ikiwa pamoja na kutoa msaada wa chakula vikiwamo unga kilo 220, maharage kilo 50 na sukari kilo 20.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment