Search This Blog
Wednesday, September 11, 2019
Kipa afariki akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa
Kipa wa timu ya taifa ya Curacao Jairzinho Pieter amefariki dunia akiwa katika kambi ya timu yake ya taifa wakati ambao ilikuwa ikijiandaa na mchezo dhidi Haiti.
Jairzinho ,31, alikuwa sehemu ya Kikosi cha Curacao kinachojiandaa mchezo wa CONCACAF Nations League dhidi ya Haiti.
Shirikisho la soka la taifa lake limeeleza kuwa Jairzinho amefariki akiwa katika hoteli ya Port-au-Prince, nchini Haiti ilipokuwa imeweka kambi timu yake ya taifa.
Waziri wa michezo wa Curacao Edwing Charles amethibitisha kuwa chanzo cha kifo cha kipa huyo wa akiba wa timu hiyo ni tatizo la moyo ambalo alikuwa nalo
Licha ya kifo hicho wachezaji Curacao walisisitiza mechi yao na Haiti ichezwe ili kutoa heshima kwa kipa wao. Mechi hiyo ilichezwa usiku wa kuamkia jana na kuisha kwa sare ya 1-1.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment