Search This Blog
Sunday, September 22, 2019
Kinga ni bora kuliko Tiba - RC Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Tellack amewaasa Wananchi wa Mkoa huo kujikita katika huduma za kukinga kuliko kutibu magonjwa ili kuondokana na gharama kubwa zinazotumika katika kutibu kwenye ngazi ya familia na Serikali.
Wito huo ameutoa wakati akiongea na Wananchi wa Shinyanga katika mji wa Kahama ikiwa ni siku ya kufunga kwa Kampeni ya Kitaifa ya ujenzi wa vyoo bora na kuvitumia kwa usahihi ” USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” iliyofanyika katika viwanja vya Majengo, Kahama.
Mhe. Zainab Tellack amesema kuwa idadi kubwa ya magonjwa ya mlipuko nchini kama vile kuhara na kipindupindu yanatokana na tatizo la kutokuwa na vyoo bora na kutonawa mikono kwa maji safi chirizika na sabuni hali inayopelekea kuingia gharama kubwa kutibu magonwa hayo.
Aliendelea kutoa wito kwa kusisitiza, ujenzi wa choo bora na matumizi sahihi utasaidia kupunguza matumizi ya dawa mara kwa mara ambayo hayana ulazima, jambo litalosaidia kupunguza usugu dawa, na madhara mengine madogo madogo yatokanayo na matumizi ya dawa.
Aidha, Mhe. Zainab Tellack ameahidi kuwa, kama Mkoa ifikapo Disemba 31 kaya zote katika Mkoa wa Shinya lazima zitakuwa na vyoo bora, na kuvitumia vyoo hivyo kwa usahihi ili kuendelea kujikinga dhidi ya magonjwa ya Kipindu pindu, kuhara na minyoo.
Kwa upande wake Mratibu wa Kampeni ya “USICHUKULIE POA, NYUMBA NI CHOO” Bw. Anyitike Mwakitalima amesema kuwa kila dakika moja Dunia inapoteza watu 4, sawa na watu 6000 kila siku, huku sababu ya vifo hivyo ikiwa kula kinyesi hali inayotokana na kutotumia vyoo na kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni, huku wahanga wakubwa wa tatizo hili wakiwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...



No comments:
Post a Comment