Search This Blog

Sunday, September 22, 2019

Afrika Kusini: Polisi wawapiga risasi watuhumiwa tisa wa ujambazi


Polisi ya Afrika Kusini wamewapiga risasi watuhumiwa tisa wa ujambazi katika mji wa Isipingo uliopo kilomita 19 kusini mwa Durban jimboni KwaZulu-Natal.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi ya mkoa Nqobile Gwala, polisi kwanza walivamia genge la watu wanane waliokuwa wanataka kuiba kwenye jengo la biashara.

Baada ya kuwaona polisi watuhumiwa hao walianza kuwafyatulia risasi, ambapo polisi nao walirejesha mashambulizi. Polisi pia wamekamata bunduki tatu, bastola sita, vilipuzi na vifaa vya kuvunjia kutoka kwa watuhumiwa waliouawa.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...