Search This Blog
Sunday, September 22, 2019
Waziri Mkuu afungua Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa hapo jana alifungua Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yaliyoanza tarehe 20 Septemba, 2019 na kutarajiwa kumalizika tarehe 29 Septemba, 2019.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo, Waziri Mkuu Majaliwa ametoa pongezi kwa Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwa kuboresha shughuli za madini kupitia kuongeza ajira na vitendea kazi kama vile magari kama njia mojawapo ya kuboresha ukusanyaji wa maduhuli.
Akielezea mafanikio ya Soko la Madini Geita tangu kuanzishwa kwake Majaliwa amesema kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa dhahabu kutoka takribani kilo 100 hadi kilo 200 na zaidi kwa mwezi na kusisitiza kuwa, tangu kuanzishwa kwa soko la madini la Geita kiasi cha kilo 1,573 zimezalishwa na kuuzwa.
Katika hatua nyingine, ameitaka Tume ya Madini kuongeza kasi kwenye ukusanyaji wa maduhuli ili Sekta ya Madini iwe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi .
Aidha, amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kuyatumia vyema masoko ya madini yaliyoanzishwa nchini na kuwataka wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha yanalindwa.
Pia, amewataka wachimbaji wa madini kutumia tafiti zinazofanywa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) kubaini maeneo yanye madini na kuanza kuchimba ili kuepuka uchimbaji wa kubahatisha.
Amesema serikali itaendelea kuboresha Sheria na Kanuni ili kuleta tija zaidi na hivyo kuwataka wananchi kuchangamkia fursa zilizopo kwenye sekta ya madini ikiwemo kutoa taarifa kwenye vyombo vya udhibiti.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment