Search This Blog

Tuesday, August 20, 2019

Simiyu yazindua Kampeni ya Nyumba ni Choo


Jumla ya kaya 6,459 sawa na asilimia tatu (3) hazina vyoo kabisa mkoani Simiyu huku kaya 6000 zikitajwa kutokuwa na vyoo kabisa.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini katika uzinduzi wa Kampeni ya Nyumba ni Choo mkoani humo na kuongeza kuwa ni aibu kwa mkoa.

Katika kuonesha kuwa kama mkoa wako tayari kufuta aibu hiyom Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka amepandisha bendera nusu mlingoti kuashiria asimilia 46.7 ya kaya zilizo na vyoo bora na kuahidi kuwa ifikapo Novemba Mosi mwaka huu mkoa huo utakuwa umehakikisha kaya zote zinakuwa na vyoo bora na hatimaye kuipeperusha bendera hiyo hadi kileleni.

Kampeni ya nyumba ni choo itafanyika mkoani Simiyu kwa takribani siku 20 katika wilaya zote za mkoa huo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...