Search This Blog

Monday, August 26, 2019

Naibu Waziri wa Nishati awasha umeme katika vijiji vinne Kilimanjaro


Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amefanya ziara ya siku mbili katika Mkoa wa Kilimanjaro, ziara iliyolenga kukagua na kuwasha umeme katika vijiji vinne ambavyo ni Roo, Msamadi vilivyopo wilaya ya Hai ,Wiri pamoja na Engaranairobi vilivyopo wilaya ya Siha.

Katika Ziara hiyo Naibu Waziri ameambatana na Meneja Mwandamizi kanda ya kazkazini Mhandisi Stella Hiza pamoja na Uongozi mzima wa TANESCO Mkoa wa Kilimanjaro.

Naibu Waziri akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Msamadi Wilaya ya Hai amesema adhima ya serekali ya awamu ya tano ni kuwasha vijiji vyote ili kuleta maendeleo kwa wananchi kwa gharama nafuu kwa bei elekezi ya shilingi 27,000 pekee.

Naibu Waziri alihitimisha mkutano kwa kutilia mkazo vijiji na vitongoji vilivyobaki kuwekwa katika awamu ya tatu mzunguko wa pili itayoanza mwaka wa fedha 2020/2021.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...