Search This Blog
Monday, August 26, 2019
Asilimia 56 ya vifo vya watoto wachanga husababishwa wakati wa utoaji huduma za Afya
Asilimia 56 ya vifo vya watoto wachanga husababishwa na magonjwa yanayotokea wakati wa utoaji huduma za Afya (Healthcare Associated Infections) katika nchi zinazoendelea.
Hayo yamesemwa na Afisa kutoka kitengo cha uhakiki ubora wa huduma kutoka Wizara Afya Dkt. Radenta Bahegwa kwenye semina ya mafunzo ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa yanayoendelea Mkoani Kagera, kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa IPC Guidline).
Alisema taarifa ya tafiti inasema kuwa asilimia 75 ya vifo hivyo vilitokea katika nchi zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo nchi ya Tanzania, huku ukosefu wa huduma ya maji safi yakutosha katika baadhi ya zahanati ikionekana ni moja ya changamoto iliyosababisha tatizo hilo la vifo.
Aidha, alisema kutofuata kanuni na taratibu za utoaji huduma kwa wagonjwa kwa baadhi ya Watoa huduma ni moja kati ya visababishi vikubwa vya vifo vya vichanga vingi katika nchi zinazoendelea, jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya Sekta ya Afya katika nchi hizo ikiwemo Tanzania.
Hata hivyo alisisitiza kuwa ni muhimu kwa Watoa Huduma kufuata misingi na taratibu za kutoa huduma kwa Wagonjwa (IPC Standard) ikiwemo kunawa mikono ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi yanayotokea wakati wa utoaji huduma kwa Wagonjwa ikiwemo vichanga (Healthcare Associated Infections).
Aliongeza kuwa kuweka mazingira safi kutasaidia kupunguza hatari za maambukizi kwa Mgonjwa au kwa Watoa huduma, pia kunaongeza hamasa ya kufanya kazi kwa bidi kwa Watoa huduma na kuvutia wagonjwa jambo litalosaidia kuongeza mapato katika Kituo cha Afya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment