Search This Blog

Tuesday, August 27, 2019

Kiswahili ni kiunganishi kati ya Rwanda na Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa lugha ya Kiswahili itakuwa ni kiunganishi kizuri katika kukuza ushirikiano na uhusiano kati ya Rwanda na Zanzibar.

Rais Dk. Shein aliyasema hayo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Eugine Kayihura ambaye alifika Ikulu kwa ajili ya kuaga.
 
Katika maelezo yake, Rais Dk. Shein alimueleza Balozi Kayihura kuwa azma ya Rwanda na Zanzibar kushirikiana katika sekta ya elimu hasa katika mafunzo ya lugha ya Kiswahili itajenga uhusiano mwema kati ya pande mbili hizo.

Rais Dk. Shein alieleza kuwa hatua hiyo itakuwa na mafanikio makubwa hasa ikizingatiwa kuwa hivi sasa lugha ya Kiswahili tayari imeteuliwa kutumika rasmi katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...