Search This Blog

Tuesday, August 27, 2019

Dkt. Mahiga akutana na Asasi ya utawala wa sheria ya Ireland


Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga amekutana na asasi isiyo ya kiserikali ya Utawala wa Sheria ya nchini Ireland ofisini kwake katika mji wa Serikali Mtumba ulioko Jijini Dodoma.

Ugeni huo ambao uliongozwa na Naibu Balozi wa Ireland nchini Bi. Brognagh Carr ulijumuisha Jaji Ailleen Donolley wa Mahakama Kuu ya Ireland, Mary Rose Gearty Mwendesha Mashtaka nchini Ireland, Kate Mulkerrins Mkuu wa Idara ya Sheria katika Jeshi la Polisi nchini Ireland. Ugeni huo pia uliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika tawi la Tanzania (WiLDAF) Anna Kulaya.

Katika mazungumzo yao wamezungumzia namna ya kuangalia jinsi ambavyo wanaweza kutumia ujuzi na utaalamu wao katika kusaidia Mahakama nchini, kuona vyanzo vya matatizo ya kijamii nchini na jinsi ya kusaidia kukakabiliana navyo na kwa pamoja kuja na mpango wa kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia nchini.

Ujumbe huo pua umejadili maeneo ambayo pande hizo mbii zinaweza kushirikiana katika harakati za kukabiliana na vitendo cya ukatili wa kijinsia na upatikanaji wa haki za kijinsia nchini.

Asasi ya Utawala wa Sheria inaundwa na wanasheria wa nchini Ireland inafanya kazi ya kukuza utawala wa sheria katika nchi zinazoendelea kwa kutumia ujuzi na wanasheria wa nchi hiyo kuhakikisha upatikanaji haki duniani na kuwezesha wananchi kuishi katika jamii ambazo hazikabiliwi na matatizo ya kutokuwa na usawa, rushwa na migogoro.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...