Search This Blog
Sunday, August 4, 2019
Dereva wa RC Mara aanguka kwa Presha
Dereva wa Mkuu wa Mkoa wa Mara amelazwa hospitali baada ya kuanguka kwa presha alipofika eneo ambapo mtoto wake (26) alipopatia ajali wakati akiendesha gari ya Mkuu wa Mkoa.
Mtoto huyo aliyechukua gari bila ridhaa ya babaye, pia amelezwa hospitali kutokana na majeraha aliyopata.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara amesema dereva huyo akipona atachukuliwa hatua kwa uzembe wa kuacha gari hadi ikachukuliwa na mwanae, na kwamba kuna uwezekano huwa anamwachia kila mara.
Ameweka wazi kuwa, mtoto huyo akipona naye atachukuliwa hatua za kisheria.
Kamanda wa Polisi amesema kuwa mtoto huyo alichugua gari hilo baada ya baba yake kuiacha nje ikiwa inaunguruma kutokana na kupata mgeni wakati alipokuwa akijiandaa kulirudisha ofisini kwa mkuu wa mkoa alipomaliza kuliosha.
Alipofika katika eneo la Kwangwa, Musoma gari ilimshinda mtoto huyo kisha ikatoka nje ya barabara na kugonga ukuta wa daraja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment