Search This Blog
Sunday, August 4, 2019
Serikali kuzilinda Taasisi za kidini
Serikali imesema itaendelea kuziunga mkono taasisi za kidini nchini ili ziweze kuleta maendeleo na kutekeleza majukumu yao vizuri ikiwa ni mdau muhimu katika maendeleo na ustawi wa nchi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa kupokea msaada wa vyerehani Tisini na Nne vyenye thamani ya Shilingi Milioni Ishirini na Nne vilivyotolewa kwa taasisi ya TAYI inayojishughulisha na kuwaokoa vijana kutoka katika tabia hatarishi ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya.
"Serikali tumekua tukipokea misaada mbalimbali kutoka katika taasisi za kidini nchini,wamekua wakisaidia visima vya maji,mashule na kubwa zaidi wanafundisha maadili ili taifa letu liwe na watu makini wanaoweza kuliletea maendeleo siku za usoni,kwa niaba ya serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani tunaahidi kuzilinda taasisi hizi ili ziweze kufanya shughuli zake bila kubughudhiwa," alisema Masauni.
Mwenyekiti wa Taasisi iliyotoa msaada huo wa vyerehani, Aref Nahdi amewaomba wananchi waliopokea mssada huo kwenda kuzitumia katika shughuli za ujasirimali akiamini watapata kipato zaidi endapo watazitumia vizuri.
"Nawaomba mkazitumie vizuri ili ziweze kuwaongezea kitu kwenye vipato vyenu,natoa wito msiende kuviuza kwani lengo lake ni kuwawezesha muwe na shughuli itakayowaingizia kipato na sisi kama taasisi tunaahidi kiasi cha Shilingi Milioni Moja kwa wale wanafunzi ishirini wa kwanza watakaotaka kujifunza ushonaji ili waweze kuzitumia vizuri," alisema Nahdi
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi waliopokea misaada hiyo ya vyerehani wameishukuru taasisi hiyo kwa kuwapa vyerehani hivyo huku waiwaomba wasichoke kuwasaidia mara kwa mara ili vijana wengi wawe na shughuli za kuzalisha kipato.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment