Search This Blog
Thursday, August 8, 2019
Aliyekuwa Rais wa Brazil kuhamishiwa Gereza la Sao Paulo
Mahakama ya juu nchini Brazil imebatilisha uamuzi wa hapo awali wa kumuhamisha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Luiz Inacio Lula da Silva kutoka kwenye gereza la muda mfupi la Curitiba anakozuiliwa na kumpeleka katika gereza la umma katika jimbo la Sao Paulo.
Lula amekuwa akizuiliwa katika gereza la Curitiba kwa zaidi ya mwaka moja. Uamuzi wa kuondoa Lula kutoka gereza hilo la Curitiba uliafikiwa juzi asubuhi huku jaji msimamizi akidai kuwepo kwa changamoto za kuweka kiongozi huyo kwenye gereza hilo kwa kuwa lilitengenezwa kuzuilia wafungwa kwa muda mfupi.
Vilevile, jaji huyo alitaja fujo ambazo hutokea kila mara baina ya wafuasi wa Lula na wapinzani wake mbele ya gereza hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment