Search This Blog
Monday, July 15, 2019
RC Zambi awaasa wastahafu kuwa na maadili
Na Ahmad Mmow-Lindi
Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amewaasa wastahafu mkoani humu wazingatie maadili mema baada ya kumaliza utumishi wa umma.
RC Zambi alitoa rai hiyo wakati wa hafla ya kuwaaga wastafu wa Jeshi la Polisi na kuwakaribisha askari wengine waliohamishiwa mkoani humu.
Hafla ambayo ilifanyika jana katika mjini Lindi, Mkuu huyo wa mkoa wa Lindi ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Lindi, alisema wastahafu wawe wa adilifu wanapoanza maisha mapya uraiani.
Alibanisha kwamba baadhi ya askari, wakiwamo maofisa baada ya kustahafu wamekuwa wakijiingiza kwenye makundi ya kihalifu. Kitendo ambacho ni kibaya ambacho hakistahili kufanywa na askari hao wastahafu ambao walipokuwa katika utumishi wa umma walikemea na kupambana kukomesha vitendo hivyo.
"Baadhi ya askari baada ya kustahafu utumishi wa umma wanajiingiza kwenye ujambazi na vitendo vingine visivyokubalika kwa mujibu wa sheria,'' alisema Zambi.
Mbali na hayo, Mkuu huyo wa mkoa alitoa wito kwa watumishi waliobado kazini kujiandaa katika maisha ya ustahafu ili watakapo maliza muda wao wa utumishi wasijiingize katika uhalifu kutokana na ugumu wa maisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment