Search This Blog

Sunday, July 21, 2019

Mbunge wa Babati Mjini kulifanyia jimbo lake makubwa katika michezo


Na John Walter, Babati

Mbali na michezo kutoa fursa ya ajira kwa wana michezo bali pia inasaidia kuwaepusha vijana na tabia ya kukaa kwenye vijiwe na hivyo kuharibu malengo katika maisha yao.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu wakati akizindua Mashindano ya Michezo mbalimbali katika mji wa Babati yaliyopewa jina GEKUL CUP 2019 huku yakisimamiwa na Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Paulina Gekul (Ccm).

DC  Kitundu amesema suala la Michezo ni miongoni mwa mambo yanayofanywa na serikali kupitia ilani ya Ccm hivyo alichofanya Mbunge Huyo ni suala ambalo wao kama serikali wanaliunga mkono kwa nguvu zote.

Amesema serikali itaendelea kusaidia jitihada za wadau mbalimbali juu ya michezo kwa kuwa  inasaidia kwa kiwango kikubwa katika  kupunguza vitendo vya uhalifu pamoja na mawazo yasiyo na maana kwa vijana.

Kwa upande wake, Mwandaaji wa Mashindano hayo Mbunge wa jimbo la  Babati Mjini Paulina Gekul amesema lengo kuu la mashindano hayo ni kuwaondolea wakazi wa Babati hatari ya kupata maradhi mbalimbali kupitia Michezo.

 Ili kufanikisha zoezi hilo, ofisi ya mbunge wa Jimbo la Babati Mjini  Paulina Gekul imetoa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya  Shilingi 10 milioni kwa timu  za vijana kwenye kata nane jimboni hapo ili kuwawezesha kushiriki Michezo.

Akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Babati waliojitokeza katika uwanja wa Kwaraa, Gekul amesema Jumla ya shilingi milioni 35 zitatumika kwa ajili ya kuendesha Michezo mbalimbali ikijumuisha Vifaa hivyo vya Michezo,zawadi zitakazotolewa zaidi ya Shilingi Milioni Kumi pamoja gharama za uendeshaji shilingi milioni kumi ambayo itafikia tamati July 27.

Mbunge huyo amesema vijana wengi wana vipaji lakini hawana mahali pa kuonyesha viapaji vyao hivyo  Michezo hiyo itakuwa ikifanyika  kila mwaka.

Aidha amesema  kwa upande wa wasanii atawapatia vifaa vya muziki ambavyo vitawawezesha kurekodi nyimbo zao kwa gharama ndogo.

Mshindano hayo yanajumuisha Michezo kumi na mbili ukiwemo mpira wa mikono kwa wanawake kwa timu sita,Volleyball timu nane,riadha,Pool tabale,kukimbiza kuku,Bao,mashindano ya kula mkate na soda,kuvuta kamba,ngoma za asili pamoja na mchezo maarufu wa mpira wa Miguu ambapo timu nane  kutoka kila kata zitachuana vikali kutafuta shilingi Laki saba,Laki tano na shilingi Laki tatu.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...