Search This Blog

Monday, July 22, 2019

Kwanini January aweke picha wakati maji yamekorogeka? - Mzee Mwinyi ahoji


Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi amefunguka kuhusua kitendo cha Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, kuweka picha aliyopiga naye katika ukurasa wake wa ‘twitter’ mara tu baada ya kutenguliwa uwaziri na Rais John Magufuli Jumapili Julai 21, ambapo amesema haikuwekwa kwa wakati sahihi.

Katika picha hiyo, ambayo January aliiweka muda mchache baada ya Rais kutengua uteuzi wake ikimuonyesha yeye na Mwinyi wamekaa kwenye viti viwili tofauti, ambapo aliandika;
“Kwa kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa. Nitasema zaidi siku zijazo.”

Mwinyi amesema hakuona ubaya wa picha ile na wala hakuchukizwa nayo kwa sababu watu wengi wanaokwenda kumuona humuomba picha ya ukumbusho lakini kilichomshangaza ni kitendo cha kutumia picha hiyo katika kipindi hichi.

“Kwa kweli sikupenda kuona picha ya namna ile katika mazingira haya, ile ni picha ya kawaida maana watu wengi wanakuja kuniona na tukishamaliza kuzungumza wanasema tupate ukumbusho na tumefanya sana kwa mtu mmoja mmoja na kwa watu wengi sana kwahiyo nimestaajabu nilipoona imewekwa wakati huu.

“Kijana yule ameandika kitabu na aliniomba nimsaidie kuandika dibaji, inawezekana alifanya kama kushukuru lakini silaumu wala sioni vibaya ila kwanini ikawe katika mazingira haya wakati maji yamekorogeka.

”Ile picha ni ya zamani lakini mambo yametokea leo na huko zamani tulikuwa na sababu ya kufanya hivyo kwasababu na mimi nilishika nafasi hii lakini pia kulikuwa na uhusiano wa kitabu chake alichokiandika maana si cha sasa hivi kiliandikwa zamani lakini kwanini ikawa sasa hivi hili kidogo limenishtua,” amesema Mwinyi.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...