Search This Blog
Monday, July 22, 2019
Q Chilla ala shavu WCB
Msanii wa Bongo fleva Rajab Kahali maarufu Harmonize ametangaza nia ya kumsaidia msanii mwenzie Aboubakary Katwila maarufu Q Chilla ili kumrudisha tena kwenye soko la muziki baada ya kupotea.
Harmonize amesema kwa kuanzia watatoa EP (albam fupi) yenye nyimbo tatu na video zake ambazo wameshirikiana kwa pamoja na wameipa jina la ‘Return of Q Chilla’ na itaachiwa Julai 22.
Akizungumza na waandishi wa habari, Harmonize amesema anamsaidia Q Chilla kwa kushirikiana na uongozi wa lebo ya WCB chini ya msanii Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz.
“Q Chilla ni msanii mkubwa hapa nchini na ndiyo chanzo cha maendeleo ya muziki wetu kwa kushirikina na uongozi wa Wasafi tumeona tushirikane na watanzania kuhakikisha kipaji chake hakipotei ili pia apate maisha mazuri na familia yake,” amesema Harmonize.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment