Search This Blog

Monday, July 22, 2019

Rais Magufuli atoa agizo kero ucheleweshaji vibali NEMC itatuliwe


Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa agizo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Goerge Simbachawene  kushughulikia kero ya ucheleweshwaji wa vibali kwa wawekezaji ili kuendana na kasi ya uchumi wa viwanda.

Amelitaka  Baraza la  la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kutochelewesha utoaji wa vibali kwa wawekezaji ili kuongeza ufanisi katika ukuaji wa uchumi wa viwanda.

“Pasiwe na ucheleweshwaji wa vibali vya NEMC kwa viwanda vyetu, sisi tunataka kuwa na viwanda vya kutosha na wawekezaji wasiwekewe vikwazo kwa visingizio vya NEMC, vibali hivi vitoke kwa sababu tunahitaji viwanda, ikiwezekana wawekeze kwanza vibali vya NEMC vitafuata baadae,”alisema Dkt. Magufuli.

Rais Magufuli amemtaka Simbachawene kusimamia kwa karibu suala hilo la ucheleweshwaji wa vibali vya Tathmini ya uharibifu wa Athari ya Mazingira vinavyotolewa na NEMC.

Rais Magufuli ameongeza kuwa fedha nyingi zinatolewa na wafadhili kwa ajili ya miradi ya mazingira lakini kumekuwa hakuna matokeo ya kuridhisha hivyo ametaka kuwepo usimamizi madhubuti wa rasilimali fedha inayoelekezwa katika miradi ya mazingira.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...