Serikali ya Uingereza inapanga kuiongezea vikwazo Iran, baada ya nchi hiyo kuiteka meli yake ya mafuta katika Ghuba ya Uajemi.
Gazeti la Daily Telegraph la Uingereza limeripoti kwamba Waziri wa Mambo ya Nje Jeremy Hunt huenda baadae hii leo, akatangaza hatua za kidiplomasia na kiuchumi zitakazochukuliwa dhidi ya Iran.
Uingereza, huenda pia ikaomba kurejeshwa upya kwa vikwazo ambavyo awali Iran iliwekewa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas ametahadharisha kwamba mzozo huo kati ya Uingereza na Iran unaweza kuongezeka.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment