Search This Blog
Sunday, June 2, 2019
Watanzania 10,000 kulipwa fidia ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi (EACOP)
Imeelezwa kuwa, jumla ya wananchi 10,000 watalipwa fidia kutokana na kupisha mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi linalotoka Uganda hadi Tanzania (EACOP), lenye urefu wa kilometa 1445.
Hayo yemesemwa tarehe 1 Juni, 2019 na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Mkoa wa Kagera lililohusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki lililofanyika wilayani Bukoba, Mkoa wa Kagera.
Kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti, Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi, Mwanamani Kidaya, Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wabunge na wawakilishi wengine wa wananchi. "Katika mwaka huu wa fedha tumetenga zaidi ya shilingi Bilioni 50.7 kwa ajili ya kazi za fidia na hatua inayofuata ni kuwataarifu wananchi waliofanyiwa tathmini na kuwaonesha stahili zao ni zipi kabla ya kuanza kulipa." amesema Dkt. Kalemani
Kuhusu ujenzi wa Bomba hilo, Dkt Kalemani amesema kuwa, matarajio ni kuanza ujenzi mwezi Septemba mwaka huu, mara majadiliano baina ya pande zinazohusika na mradi huo kukamilika na mradi unatarajiwa kukamilika baada ya miaka mitatu.
Kuhusu mradi huo, Dkt Kalemani amesema kuwa, utaajiri watanzania takribani 10,000 wakati wa ujenzi na baada ya ujenzi watanzania zaidi ya 200 wataajiriwa na kwamba Bomba litakalojengwa litakuwa na uwezo wa kusafirisha mapipa laki 216,000 kwa siku na kila pipa litalipiwa Dola 12.2 kama ushuru.
Alisema kuwa, gharama za mradi ni USD bilioni 3.5 na kwa upande wa Tanzania Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ndilo litakashiriki katika ujenzi wa mradi huo kwa niaba ya Serikali.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amewapongeza wataalam kutoka Tanzania wanaoshiriki katika majadiliano ya mradi huo ambayo kwa sasa yamefikia zaidi ya asilimia 80 hali itakayowezesha pande zinazohusika na mradi kuanza utekelezaji wa mradi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment