Search This Blog

Sunday, June 2, 2019

China kuongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani


China imetangaza kuongeza ushuru wa bidhaa za mabilioni ya dola kutoka Marekani wakati ikijitayarisha kuchapisha orodha mbaya ya kampuni za kigeni hatua ambayo wachambuzi wanasema inalenga kuiadhibu Marekani na kampuni za kigeni zinazoacha kufanya kazi na kampuni kubwa ya simu ya China, Huawei.

Hatua hiyo ya China inalenga kuziongezea ushuru bidhaa za Marekani zenye thamani ya dola bilioni 60, kuanzia asilimia 5 hadi 25 na inakuja baada ya Washington kuongeza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 200.

Hatua hizo za kulipiziana kisasi zimeongezeka wiki za karibuni baada ya Marekani kuiorodhesha kampuni ya Huawei ya China katika orodha ya kampuni zinazotishia usalama wa taifa.

Mataifa hayo mawili yamewekeana nyongeza ya ushuru kwenye biashara baina yao kwenye bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 360.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...