Search This Blog
Sunday, June 2, 2019
Neymar ashutumiwa kwa ubakaji
Mwanamke mmoja amemshutumu Neymar kwa kumbaka wakati mchezaji soka huyo maarufu wa Brazil akiwa amelewa katika hoteli moja mjini Paris, Ufaransa.
Hayo ni kulingana na ripoti ya Kituo cha Polisi cha Sao Paulo iliyoonekana na shirika la habari la Reuters.
Shutuma hizo ni za hivi karibuni dhidi ya mwanasoka huyo wa Brazil, ambaye mwezi uliopita alivuliwa unahodha wa timu ya taifa kufuatia matukio ya utovu wa nidhamu, hatua iliyomchafulia sifa.
Kulingana na ripoti ya polisi, mwanamke ambaye hakutajwa jina aliwaambia wachunguzi wa Sao Paulo kwamba alikutana na Neymar kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na mwanasoka huyo alipendekeza wakutane mjini Paris, ambako anachezea timu ya Paris St Germain.
Msaidizi wa Neymar alimtumia tiketi za ndege mnamo Mei 15. Wawakilishi wa Neymar bado hawajatoa tamko lolote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...

No comments:
Post a Comment