Search This Blog
Sunday, June 2, 2019
Mitandao ya kijamii ya wanaotaka kwenda Marekani kuchunguzwa
Wote wanaotuma maombi ya kupata Visa kueleka nchini Marekani sasa watahitajika kutoa majina yao ya mitandao ya kijamii, anwani zao na nambari za simu katika sheria mpya zilizowekwa.
Kulingana na sheria mpya za idara ya maswala ya kigeni, wanaotuma maombi ya Visa watahitajika kutoa majina yao ya mitandaoni mbali na anwani za miaka mitano pamoja na nambari za simu.
Wakati sheria hiyo ilipopendekezwa mwaka jana, mamlaka ilikadiria kwamba itaathiri takribani watu milioni 14.7 kila mwaka.
Hatahivyo baadhi ya wanadiplomasia na maafisa wanaotuma maombi ya kibali hicho huenda wakasamehewa.
Hatahivyo watu wanaoelekea Marekani kufanya kazi ama kusoma watalazimika kutoa habari zao .
''Tunajaribu kutafuta mikakati ya kuimarisha ukaguzi wetu ili kuwalinda raia wa Marekani , huku tukiunga mkono wale wanaosafiri kihalali'' , ilisema Idara hiyo.
Awali , ni watumaji maombi waliohitaji ukaguzi wa zaidi -kama vile watu waliosafiri katika maeneo yanayodhibitiwa na magaidi -ambao wangelzimika kutoa data hiyo.
Lakini asasa wanaotuma maombi watalazimika kutoa majina ya akaunti zao katika mitandao ya kijamii, mbali na kutoa maelezo ya akaunti zao katika mtandao yoyote.
''Mtu yeyote atakayedanganya kuhusu matumizi yao ya mitandao ya kijamii huenda akakabiliwa na adhabu kali ya uhamiaji'', kulingana na afisa aliyezungumza na The Hill.
Rais Donald Trump
Utawala wa rais Donbald Trump ulipendekeza sheria hizo mnamo mwezi Machi 2018.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment