Search This Blog

Sunday, June 23, 2019

Serikali yaja na mikakati ya kuwaendeleza wabunifu mbalimbali nchini

Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mh Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli imejipanga kuwaendeleza wabunifu mbalimbali nchini kwa kuwawezesha kupitia mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ili waweze kutoa mchango chanya katika maendeleo ya Nchi.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde katika maonesho ya wabunifu wa Sayansi yalioenda sambamba na maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wanataaluma wa College(Ndaki) ya Sayansi ya Asili na Hisabati,Chuo kikuu cha Dodoma.

“Sayansi na Utafiti ni mambo muhimu sana katika Uchumi wa Viwanda,wabunifu hawa niliowaona leo wana mchango mkubwa sana katika kuleta tija kupitia uchumi wa Viwanda,hivyo ni wajibu wa Serikali kuhakikisha inawasimamia  na kuwaendeleza ili waweze kufikia malengo”Alisema Mavunde

Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Rasi(Principal) wa Chuo cha Sayansi ya Asili na Hisabati Prof Said Vuai ameeleza malengo makubwa ya Chuo hicho ni kutoa wahitimu ambao watakwenda kutatua matatizo katika jamii na ndio maana wanawalea na kuwaanda kuja kuitumikia jamii katika kuboresha huduma katika jamiina kuiletea maendeleo.


Wabunifu waliotoa fora ni wale wanaotumia maganda ya machungwa na malimao kutengeneza dawa ya kuua minyoo ya kuu na wengine waliokuja na kifaa maalum cha kuzuia kuiba gari.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...