Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema, mkuu wa majeshi wa nchi hiyo Searre Mekonnen, amepigwa risasi na bado hali yake haijulikani.
Waziri mkuu Ahmed ametoa tamko hilo kwa njia ya televisheni, muda mfupi baada ya jaribio la mapinduzi, kwenye eneo la Amhara.
Hata hivyo, maelezo zaidi hayakutolewa juu ya kupigwa risasi kwa mkuu huyo wa jeshi. Awali ubalozi wa Marekani ulionya mara kadhaa juu kusikika milio ya risasi katika mji mkuu Adis Ababa, na machafuko katika mji muhimu wa Amhara, Bahir Dar.
Ofisi ya waziri mkuu haikutoa taarifa yoyote juu ya watu waliohusika na jaribio hilo.
Tangu alipoingia madarakani mwezi Aprili mwaka 2018, Waziri mkuu Abbiy Ahmed amekuwa akifanya juhudi za kukomesha mabaki ya utawala wa mkono wa chuma kutoka kwa watangulizi wake.
Amefanikiwa kupambana na migogoro baina ya makabila mengi ikiwemo ya kugombea ardhi iliyokuwa ikisababisha machafuko nchini humo.

No comments:
Post a Comment