Search This Blog

Sunday, June 23, 2019

Balozi Sokoine aongoza zoezi la Ukusanyaji mifuko ya Plastic Dodoma



Na.Lulu Mussa,OMR

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine amewaongoza Watumishi wa Ofisi yake kwenye zoezi la usafi katika eneo la Makulu, jijini Dodoma ikiwa sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

Katika zoezi hilo lililohusisha pia Baraza Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Halmashauri ya Jiji la Dodoma na wananchi, Balozi Sokoine alisema zoezi hilo litakuwa endelevu ili kuhakikisha mazingira yanatunzwa.

Aliwataka wananchi kuendelea na utamaduni wa kukusanya mifuko ya plastiki na taka kila wanapozikuta kwenye mazingira yao ili kuhakikisha kuwa hakuna takataka zinasambaa na kusababisha uchafuzi wa mazingira.

“Eneo hili tumeona lina mifuko mingi ya plastiki hivyo tumekuja hapa katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kukusanya mifuko hii pamoja na kuelimisha wananchi juu ya katazo la mifuko ya plastiki na matumizi ya mifuko mbadala,” alisema. Balozi Sokoine.

Alisema katika zoezi hilo baada ya kukusanya mifuko hiyo ya plastiki na takakata kwa ujumla zitapimwa ili kujua zimepatikana kiasi gani na kufanya utaratibu wa kuziteketeza ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Patrobas Katambi alipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuandaa zoezi hilo la usafi katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

Mhe. Katambi alisema kuwa katazo la mifuko ya plastiki litasaidia kufanya mazingira yawe salama na hivyo kuepusha wanadamu kuwa katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali endapo itazagaa hovyo.

“Ndugu zangu mazingira yakiwa si salama hata sisi tutakuwa hatarini kupata magonjwa ambukizi na nyemelezi kwa mfano magonjwa kama kansa husababidhwa na hii mifuko ya plastiki na vilevile yanaua viumbe hai mbu wanazaliana,” alisema

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...