Search This Blog
Saturday, June 1, 2019
RC Makonda afuturisha wenye ulemavu Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda hapo jana amefuturisha maelfu ya watu wenye ulemavu na wasiojiweza kama sehemu ya sadaka yake ya Ramadhani.
Katika futari hiyo RC Makonda amewapa hadhi ya juu watu wenye walemavu baada ya kuwaalika watu mashuhuri nchini na kuwapa jukumu moja la kuhakikisha wanahudumia watu wenye ulemavu vyakula, vinywaji na kuwasikiliza shida zao jambo ambalo walemavu wamelizungumzia kama heshima ya kipekee wamepatiwa.
Aidha RC Makonda amewahimiza wananchi kuwa na moyo wa upendo na kusaidia makundi ya wasiojiweza kwakuwa anaamini kwa kufanya hivyo watachuma baraka.
Pamoja na hayo RC Makonda amewaomba wananchi kuliombea Taifa na Viongozi ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Magufuli ambae amekuwa mtetezi wa wanyonge na mpiganaji wa maendeleo kwa maslahi ya wote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...



No comments:
Post a Comment