Search This Blog

Saturday, June 1, 2019

Mratibu wa Mkutano wa Trump na Kim auawa kwa kupigwa risasi


Mjumbe maalumu wa mazungumzo kati ya Korea Kaskazini na Marekani, Kim Hyok Chol ameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kushindwa kwa mkutano wa pili wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un na Rais Donald Trump.

Kwa mujibu wa Gazeti la Chosun Ilbo limeandika Chol aliyeuratibu mkutano huo wa Hanoi na kumsindikiza Kim kwenye treni yake binafsi ameuawa kwa kupigwa risasi kwa kile kinachotajwa kumsaliti kiongozi huyo wa juu baada ya kufanikiwa kuishawishi Marekani wakati wa majadiliano ya kabla ya mkutano huo wa mwisho.

Gazeti hilo lililonukuu chanzo ambacho hakikutajwa limesema Chol, aliuawa Machi katika Uwanja wa Ndege wa Mirim pamoja na maafisa wanne waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje baada ya uchunguzi. Mkalimani wa Kim kwenye Umoja wa Mataifa naye ametiwa kizuizini baada ya kufanya makosa kwenye mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...