Mwendesha mashtaka mkuu Al Waleed Sayyed Ahmed amewaambia waandishi wa habari kwamba Bashir anakabiliwa na mashtaka ya rushwa na kumiliki fedha za kigeni kinyume cha sheria.
Hayo yanatokea baada ya zaidi ya miezi miwili tangu jeshi lilipomwondoa Bashir madarakani kufuatia maandamano makubwa ya kitaifa yaliyopinga utawala wake. Siku ya Alhamisi, afisa mmoja alinukuliwa na shirika la habari la Sudan, SUNA, akisema Bashir anakabiliwa pia na mashtaka ya kuamuru hali ya dharura nchini Sudan.
Mnamo mwezi Aprili, mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alisema fedha zaidi ya dola milioni 113 zilikamatwa kutoka kwenye makazi ya al-Bashir. Jenerali Burhan amesema polisi na wanajeshi na mawakala wa usalama walipata kiasi cha Euro milioni saba , Dola za Kimarekani 350,000 na Pauni za Sudan milioni moja na tano.
Omar al Bashir alipotangaza hali ya dharura mnamo Februari 22 katika jitihada za kuyazima maandamano yaliyoanza kutoka mwezi Desemba, Bashir alitoa alipitisha amri kwamba ni kinyume cha sheria kwa mtu kuwa na fedha za kigeni zaidi ya dola 5,000.
Mwezi uliopita, mwendesha mashtaka mkuu Ahmed aliamuru Bashir ahojiwe kuhusu tuhuma za utakatishaji fedha na kufadhili ugaidi. Mnamo mwezi Mei, mwendesha mashtaka huyo alisema Bashir atashtakiwa kwa mauaji ya waandamanaji waliokuwa wanaipinga serikali yake jambo lililosabisha kuondolewa kwake madarakani.
Ahmed amesema watuhumiwa wengine waliotumikia chini ya utawala wa Bashir bado wanachunguzwa. Ingawa hakuwataja majina lakini alisema tuhuma dhidi yao ni kuhusu umilki wa ardhi.
Maandamano dhidi ya utawala wa Bashir yalianza tarehe 19 Desemba baada ya serikali yake kupandisha bei ya mkate. Omar al Bashir aliondolewa madarakani na jeshi tarehe 11 Aprili baada ya maelfu ya waandamanaji wakiongozwa na muungano wa vyama vya watu stadi kupiga kambi mbele ya makao makuu ya jeshi katikati ya mji mkuu Khartoum kuanzia Aprili 6. Kwa sasa anazuiwa kwenye gereza la Kober.
Chanzo: AFP
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment