Search This Blog

Monday, June 3, 2019

Dk. Kalemani atoa agizo TANESCO


Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhakikisha mitaa yote kwenye majiji, inapatiwa umeme ifi kapo Juni 30, mwaka huu.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya kufanya ziara kutembelea maeneo ya Mkonze na Ntyuka katika Jiji la Dodoma, ambayo yana nyumba ambazo hazijaunganishiwa umeme.

Dk Kalemani alisema mitaa yote katika jiji hilo, inatakiwa kuwa na umeme ifikapo tarehe hiyo, kwani maeneo hayo yana kero kubwa ya kupata umeme ijapokuwa yapo jijini.

Alisema maeneo hayo lazima yapatiwe umeme haraka ili yafanane na hadhi ya jiji. Dk Kaleman alitaka wataalamu kutoka Tanesco kutokataa malipo ya wananchi, wanaotaka kuunganishiwa umeme, bali wanapaswa kuyapokea malipo hayo na kuharakisha kuwasambazia umeme wateja hao.

Kabla ya kufanya ziara hiyo, Dk Kalemani akizungumza katika kikao na watendaji wa Tanesco na kuwataka kushughulikia kwa haraka suala la kuwaunganishia umeme wananchi waliolipia.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...