Search This Blog

Sunday, May 26, 2019

Waziri Lukuvi azindua mpango kabambe uendelezaji mji Tabora


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amezindua Mpango Kabambe wa Uendelezaji Mji wa Tabora wa miaka ishirini na kuzitaka mamlaka husika wakiwemo Madiwani kuhakikisha wanasimamia vyema mpango huo ili kuleta matokeo chanya.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika mkoani Tabora jana Waziri Lukuvi alisema kazi kubwa baada ya kuzinduliwa Mpango Kabambe ni kwa wahusika kusimamia mpango huo kwa kufuata sheria na kuacha tamaa ya kuwasikiliza baadhi ya watu wenye vyeo wanavyotaka wakati wa kutekeleza. " Utekelezaji wa Mpango Kabambe niliouzindua usiangalie vyeo, pesa au ukubwa wa mtu bali ufuate sheria na msipofanya hivyo hamtapanga miji na kazi yote itaharibika" alisema Lujuvi.

Amewataka Madiwani kote nchini katika halmashauri mbalimbali kutumia vikao kushughulikia masuala ya ardhi ikiwemo utekelezaji mpango kabambe na kuacha kutumia maamuzi binafsi ya viongozi jambo linaloweza kuchangia uwepo wa migogoro ya mara kwa mara.

Kwa mujibu wa Lukuvi, mpango uliozinduliwa katika Manispaa ya Tabora ambao unaanzia mwaka 2015 hadi 2035 utapunguza migogoro ya ardhi na kuchochea utekekezaji wa malengo ya serikali kuekekea uchumi wa kati wa viwanda na kubainisha kuwa hali hiyo inajidhihirisha katika mpango huo ambapo asilimia kumi ya ardhi imepangwa kwa matumizi ya viwanda.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amezitaka taasisi mbalimbali zinazotoa huduma kuzingatia mpango kabambe wakati wa utekekezaji kazi zao na kuacha kuharibu miundo mbinu kama vile ujenzi wa miundombinu ya maji na kusisitiza kuwa lazima wakati wa ujenzi wake kuwe na matoleo ya njia za maji.

Akizungumzia uendelezaji Mji wa Tabora, Lukuvi alisema kutokana na mpango huo Kabambe uliozinduliwa sasa thamani ya maeneo ya mji huo imepanda hivyo wamiliki wake ni vyema wakaitumia fursa hiyo kujiendeleza kiuchumi.

http://bit.ly/2QmTTFX

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...