Search This Blog
Sunday, May 26, 2019
Asilimia 80 ya kaya Mkoani Kagera kuwa na choo bora ifikapo June 2021
Na Clavery Christian Bukoba.
Mkuu Wa Mkoa Kagera brigedia jenerali Marco Elisha Gaguti amesema kuwa Mkoa kwa kushirikiana na wizara ya afya umejipanga kutokomeza kaya zote ambazo hazina vyoo kabisa ifikapo 30 August 2019.
Gaguti amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira yenye kauli Mbiu isemayo "usichukilie poa nyumba ni choo" ambapo amesema kuwa kila kaya katika mkoa huu lazima iwe na choo na kukitumia hatua ambayo itasaidia kuondoa asilimia 5% ya kaya ambazo kwa sasa hazina vyoo kabisa.
"Kampeni hii haitakuwa na maana endapo baadhi ya tabia kama vile kuchimba dawa njiani ovyo zikiacha na bahati nzuri Mkoa wetu Wa Kagera una vyoo katika maeneo yaliyopo kando ya barabara kuu za bukoba, nyakanazi na bukoba, mtukula" alisema Gaguti.
Rc Gaguti amewataka wakuu wote wa wilaya za Mkoa Kagera kuanza kusimamia agizo hili ili kuweza kuzuia magonjwa ya kuambukiza kama vile kuhara, kuhara damu, kipindupindu na minyoo.Kampeni hii ya taifa ya usafia Wa mazingira itaongozwa na Msanii Wa mziki Wa bongo fleiva Bw, Mrisho Mpoto kutoka dar es salaamu.
http://bit.ly/2wkzPKZ
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment