Search This Blog

Sunday, May 26, 2019

Kauli ya Umoja wa Ulaya kuhusu kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Uingereza


Umoja wa Ulaya umesema kuwa kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Uingereza hakutobadili chochote kwenye msimamo wake wa makubaliano yaliyofikiwa kuiwezesha Uingereza kujiondoa kwenye Umoja huo.

Msemaji wa Rais wa Kamisheni ya Umoja huo, Jean-Claude Junker amesema ameupokea uamuzi wa May kwa masikitiko makubwa lakini baraza la viongozi wa Umoja lilikwishaweka msimamo wake kuhusu makubaliano ya Brexit.

Theresa May alitangaza kujiuzulu baada ya kushindwa kuwashawishi Wabunge kuunga mkono mpango wa kuiondoa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya, Brexit.

http://bit.ly/2wjiylt

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...