Search This Blog
Tuesday, May 28, 2019
Waziri Biteko: Mchango wa sekta ya madini katika pato la taifa umeimarika
Waziri wa madini Mhe.Doto Biteko amesema mchango wa sekta ya madini katika pato la taifa umeimarika na kufikia asilimia 5.07 suala ambalo limechangiwa na kuimarika kwa usimamizi wa shughuli za madini kwa kudhibiti utoroshwaji na kuimarisha ukaguzi katika sehemu za uzalishaji katika biashara ya madini sambamba na kuongezeka kwa mrabaha na kuanzishwa kwa ada ya ukaguzi masuala ambayo yametokana na marekebisho yaliyofanywa katika sheria ya madini ya mwaka 2017.
Waziri Biteko ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20 ambapo amesema uelewa kwa wadau wa sekta ya madini na uwazi katika shughuli zao umeongezeka ambapo mpaka mwezi machi mwaka huu wizara imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 244.25 sawa na asilimia 78.64 ya fedha iliyopangwa sh bilioni 310.59 huku akivitaja vipaumbele kwa mwaka ujao ikiwa ni kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kutokana na madini na uanzishwaji na usimamizi wa masoko ya madini.
Wakichangia bajeti hiyo baadhi ya wabunge licha ya kutambua jitihada zinazofanyika lakini wamesema kuna haja ya kuongezwa kwa watendaji kutokana na kuonekana wachache lakini pia kuwawekea wachimbaji wadogo mazingira ya uchimbaji ili waweze kunufaika ikiwemo kuwaondolea tozo ambazo si za lazima.
Nao baadhi ya wabunge wameishauri serikali kuwekeza zaidi katika mradi wa Liganga na Mchuchuma unakamilika na kuanza kufanya kazi ili kuleta tija kwa taifa.
Akisoma hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni katika wizara hii Mhe.John Heche mbunge wa Tarime imeitaka serikali kulieleza bunge juu ya fidia watakayopewa kwa wananchi walioathiriwa na utiririshaji wa maji yenye sumu kutoka mgodi wa North Mara baada ya kuthibitishwa na kamati zilizoundwa kuchunguza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment