Search This Blog

Tuesday, May 28, 2019

Afanya mauaji ya watu watatu na kisha kujiua


Michael John, mkazi wa Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro amejiua kwa kunywa sumu baada ya kudaiwa kufanya mauaji ya watu wengine watatu ambao ni wanawake akiwemo mke wake aliyekuwa mjamzito kwa kuwakata kata kwa mapanga kwa kilichodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa amesema awali walipokea taarifa toka kwa mkazi wa kijiji hicho Salehe Seif akiripoti tukio la kuuawa kwa mkewe Salma Mkami (52)na mwili wake kukutwa jirani na nyumbani kwake, baada ya usiku kabla ya tukio kuomba ruhusa ya kwenda kumsindikiza jirani yao Bi.Leonora Ernest aliyekuwa mjamzito, ambaye  ni mke wa mtuhumiwa lakini hakuonekana.

Kamanda Mutafungwa akasema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na akatoa wito kwa jamii kuacha wivu unaosababisha wafanye vitendo vya kikatili.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...